Wednesday 1 June 2016

Zitto Kabwe atuma ujumbe huu mzito kwa Rais Dkt.Magufuli.


Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa wao kama upinzani wanamuunga mkono Rais Magufuli jinsi anavyopambana na ufisadi, wakwepaji kodi, ubadhirifu, uvivu na uzembe lakini watampinga Rais Magufuli

kwa nguvu zao zote kutokana na kitendo cha Rais kutaka kupambana na demokrasia nchini.

Mhe. Zitto Kabwe aliandika haya kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema hawatakubali kuona wanarudishwa nyuma au kuona misingi ya taasisi za uwajibikaji zikibomolewa.

"Rais Magufuli tunakuunga mkono kwa dhati kupambana dhidi ya ufisadi. Tunakupinga kwa nguvu zote kupambana dhidi ya demokrasia. Kuanzia mwanzo tumekuunga mkono dhidi ya ukwepaji kodi, ubadhirifu, uvivu na uzembe. Tangia mwanzo tulionya kuwa ni lazima udhibitiwe na Bunge ili ufanye kazi kwa mujibu wa Katiba. Hivi sasa wewe Rais ndio unaendesha Bunge kwa remote control. Tutakupinga kuturudisha nyuma. Hutafanikiwa kamwe kubomoa misingi ya taasisi za uwajibikaji tulizoanza kuzijenga". Alisema Zitto Kabwe.

Mbali na hilo Zitto Kabwe alisema Tanzania inataka uongozi madhubuti na siyo utawala wa imla na kudai watanzania hawatakubali kurudi nyuma katika utawala wa imla.

Narudia nukuu muhimu sana " ukitaka kutawala tawala peke yako. Ukitaka kuongoza ongoza na wenzako". Rais Magufuli Tanzania inataka Uongozi madhubuti na sio utawala wa imla. Huko tumeshatoka na Watanzania hawatakubali kurudi huko". Aliongeza Zitto Kabwe



USISAHAU KULIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA,KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment