Tuesday 26 July 2016

CHADEMA watoa malalamiko haya kuhusu CCM kufanya mikutano bila kujali zuio.


Chama cha Demokrasia na maendeleo nchini  CHADEMA mkoani Tabora kimelalamikia kitendo cha baadhi ya wabunge na wanasiasa wa chama Tawala kuendelea kufanya mikutano ya kisiasa licha ya zuio lililotolewa na serikali huku jeshi la polisi likifumbia macho hatua hiyo inayodaiwa  kuwa ni upendeleo nje ya utawala bora.

Baadhi  ya  viongozi wa  Chadema  wamekutana   katika  ofisi za Chama  hicho  wilayani Igunga ikiwa ni sehemu  ya  ziara  ya  kukiimarisha chama chao kwa kufanya  mikutano  ya ndani.

Kuzuiwa kwa mikutano  ya hadhara kwa vyama vya Siasa nchini  bado inaonekana  kuwa  mwiba na kudai  kwamba inabana Uhuru wa kuikosoa Serikali awamu  ya  tano  kutokana  na  mwenendo  wake tangu  iingie  madarakani.

Licha  ya  kuamini  kwamba  huu ni  muda  wa  kuwatumikia  wananchi kwakile  walichoahidiwa  kwenye  kampeni  za  uchaguzi  mkuu  wa  mwaka  jana, lakini Chadema imejenga  imani  kubwa  ya  kutaka  uhuru  zaidi  wa  kukutana  na  wananchi  kwenye  majukwaa  ili  wapate  fursa  ya  kuelezea  madhaifu  ya  Serikali na ikibidi  kutoa  ushauri katika  kutatua kero zinazowakabili  wananchi.

No comments:

Post a Comment