Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amefanya mabadiliko ya watendaji wakuu katika sekta za misitu na wanyamapori, kwa lengo la kuongeza ufanisi wa sekta hizo katika kuchangia pato la taifa.
Akitangaza mabadiliko hayo mjini Dodoma, Waziri Maghembe amesema kwa upande wa misitu mabadiliko hayo yatahusisha viongozi wa wakala wa misitu, na wasimamizi wa misitu katika kanda zote nchini.
Aidha, kwa upande wa wanyamapori na uhifadhi kwa ujumla, Profesa Maghembe amebainisha kuwa, sekta hizo zimebadilishiwa pia viongozi wake, lengo likiwa ni lilelile la kuhakikisha kunakuwepo na matokeo chanya ya utendaji kazi.
Pamoja na mambo mengine, waziri huyo wa Maliasili na Utalii, alichukua wasaa huo kufafanua kuwa katika mwaka huu mpya wa fedha, hakutakuwepo mabadiliko yoyote ya utoaji wa vibali vya uvunaji wa miti, lakini akasema tatizo lililopo ni mahitaji kuzidi uwezo.
No comments:
Post a Comment