Watuhumiwa 1,065 wa makosa mbali Mbali ya Uhalifu ikiwemo ya Unyang’anyi wa kutumia silaha, wizi pamoja na Uporaji wametiwa mbaroni na katika Operesheni ya kupambana na matukio ya Uhalifu jijini dar es salaam,
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna wa polisi Simon Siro amesema vijana wanane wa Uporaji wa Simu na Mikoba ya kina mama kwa kutumia Pikipiki katika maeneo ya jiji ni miongoni mwa waliotiwa mbaroni pamoja na kukamata simu za mkononi 12 ambazo ziliporwa na watuhumiwa hao.
Aidha jeshi hilo limesema katika zoezi la uhakiki wa silaha ,katika mkoa wa dsm watu waliojitokeza walikuwa 11,602 silaha zilizohakikiwa zikikuwa 14,107,kati ya hizo pistol zilikuwa 5,073,short gun 4,707, riffle 2,974 huku zaidi ya silaha 66 zilisalimishwa baada ya wamiliki wake baadhi yao kutokuwa na uwezo wa kumiliki, kufariki dunia na kushindwa kulipia ada ya umiliki ambapo pia jeshi limetoa ilani kwa wale wanamiliki kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment