Friday 22 July 2016

Katiba Mkuu Chadema Dkt Vicent Mashinji atoa mbinu hizi kwa vijana wa CHADEMA kushinda Uchaguzi 2020.


Katibu Mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dkt Vicent Mashinji amewataka vijana wa Bavicha kutokuwa wazembe wakufikiria bali kujipanga kwa ajili ya kushika dola mwaka wa uchaguzi mkuu 2020 huku akiwapatia kanuni za kushinda uchaguzi huo.

Akizungumza na vijana hao jana jijini Dar es salaam Mashinji aliwaambia vijana hao chama chao kimejipanga kushika dola hivyo wao kama vijana wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya kufanya uchaguzi na kuwatambua wanachama hai, pia kuhakikisha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa vijana wanashiriki nafasi mbali mbali na kushinda

”Nataka niwape majukumu matatu ambayo mkiyafanya hayo 2020 tutashinda nakutangazwa, moja hakikisheni tunaingiza wanachama wapya na kuwahakiki walio hai, nendeni 2019 kwenye serikali za mitaa vijana mgombee na tupate viongozi ngazi ya chini viijana wasomi, na tatu kwa mwaka huu kila kijana ajue nafasi zitakozogombewa katika eneo lake hiyo itatusaidia kushinda nafasi nyingi za madiwani  kwa Tanzania bara na visiwani  na haya ndiyo majukumu makubwa ninayowapatia”   Alisema Mashinji.

Pamoja na hayo aliwataka vijana hao kuendelea kupigania haki za wanyonge na kushinda vita ya demokrasia bila kuvunja sheria huku akiwaasa kuwa askari mzuri na shujaa ni yule anayepambana bila risasi.

”Askari mzuri ni yule ashindaye vita bila kutumia risasi zake, mkawe mabalozi wa kuwatetea wanyonge na haki zao, msiwe waoga kudai katiba ya wananchi, pia kuna watu Geita, Shinyanga na Simiyu tunataarifa wanapigwa kisa itikadi ya upinzani wa vyama hivyo kama vijana mnatakiwa mpaze sauti kwa ajili yao”. aliwaambia Mashinji.

Hata hivyo Mashinji aliwaasa vijana hao kuwa wapole na kusubiri maamuzi ya viongozi wa chama kwani yanabusara. Aidha aliwapongeza vijana hao kwa kuwa na umoja wa kupigania haki na misingi ya demokrasia.

Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Patrobas Katambi alimweleza Katibu huyo wa chama kuwa wao wapo tayari kwa pambano japo wanasikiliza na kutii kauli ya chama hivyo wao  watatoa msimamo wao.

”Sisi vijana tupo tayari miili yetu ilale makaburini na tukumbukwe kama mashujaa waliokufa wakipigania haki, tumesikiliza maagizo ya viongozi wetu lakini pia sisi leo tutatoa msimamo wetu”.- Katambi

USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUTU FOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment