Wednesday 21 October 2020

Tetesi zote za soka Ulaya

 


Tottenham wanajiandaa kumuongezea Son Heung-min mshahara hadi pauni 150,000 kwa wiki ili kumshawishi mshambuliaji huyo raia wa Korea Kusini mwenye umri wa miaka , 28, akubali kusaini kuongezwa kwa mkataba wake. (Mail)

Mshambuliaji wa Southampton na England Danny Ings, 28, anakaribia kusaini mkataba utakaomuongezea muda katika klabu ya St Mary huku Tottenham nao wakiwa na nia ya kumnunua (Athletic - subscription required)

Liverpool wanamtaka Ben White
Maelezo ya picha,

Liverpool wanamtaka Ben White

Liverpool wanamtaka difenda Muingereza anayechezea Brighton Ben White baada ya Leeds United kushindwa kusaini nae licha ya kwamba waliweka dau la kumnunua mara tatu kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 tu msimu huu. (Football Insider)

Arsenal ilifanya dau la kumsaini winga wa Ureno Joelson Fernandes anayechezea timu ya Sporting Lisbon akiwa na umri a miaka 17 wakati wa dirisha la uhamisho la msimu uliopita . (Football London)

Meneja wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri anakaribia kabisa kupata kazi klabu ya Fiorentina iwapo wataamua kumfukuza Giuseppe. (Calcio Mercato - in Italian)

Manchester City wako wazi kumpokea Pablo Zabaleta anayerejea katika klabu hiyo kuchukua wadhifa ambao sio wa kimchezo kufuatia kustaafu kwa Muagentina huyo mwenye umri wa miaka 35-wiki iliyopita. (Mail)

Barcelona wanataka kumruhusu mshambuliaji wa mbele wa Mfaransa Ousmane Dembele, 23, na mshambuliaji wa Denmark Martin Braithwaite ,29, kuondoka , ili kutoa fursa kwa wachezaji wawili wa safu ya mashambulizi wa Uholanzi - Memphis Depay wa Lyon, 29, na Myron 19 AZ Alkmaar (Todofichajes - in Spanish))

Juventus wanaimani kuwa mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala,26, atasaini kurefushwa kwa mkataba wake. (Tuttosport - in Italian)

No comments:

Post a Comment