Friday 29 July 2016

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atembelea Hospital ya Ocean Road na kutoa kauli hii.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ina mpango wa kununua mashine mbili za mionzi katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam ili kupunguza changamoto inayowakabili wagonjwa wa saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Kuwepo kwa mashine hizo mbili kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa saratani katika hospitali hiyo.

Akizungumza wakati alipotembelea Taasisi ya Saratani Ocean Road na kujionea hali halisi inayoendelea katika taasisi hiyo na kuzungumza na baadhi ya wagonjwa, Makamu wa Rais amesema amejionea changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa dawa na uhaba wa mashine za mionzi ambapo ameahidi Serikali itajitahidi kuondoa changamoto hizo kwa haraka.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk Diwani Msemo amekiri kuwepo kwa changamoto ya vifaa tiba katika taasisi hiyo, hali inayochelewesha huduma kwa wagonjwa.

No comments:

Post a Comment