Monday, 8 August 2016

Kata ya Mabwepande jijini Dar es salaam yavamiwa kwa vitendo vya ubakaji na kutobolewa macho.

Maeneo ya Mji Mpya kata ya Mabwepande wilayani Kinondoni jijini Dsm yamegubikwa na Vitendo vya mauaji pamoja na Vitendo vya Ubakaji kwa Kina Mama na watoto ambapo katika kipindi cha wiki moja watu watano wameuwawa wakiwemo wanawake wawili na mtoto mwenye Umri wa miaka minne  baada ya kubakwa na kuuwawa kwa kutobolewa macho.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mitaa na Kata imekutana leo pamoja na wananchi kujadili na kuchukua hatua kutokana na Hofu iliyotanda hasa nyakati za jioni na Usiku kutokana na mapori ambayo yanadaiwa kuwa vyanzo vya matukio hayo.
M/kiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni diwani wa kata ya Mabwepande amesema maauaji hayo ya Mfulurizo yanatokana na mapori ambayo wamiliki wake kwa muda mrefu wameyatelekeza hivyo wahalifu wamekuwa wakiyatumia kuvamia watu,kuwabaka na kuwapora pikipiki na kujificha katika mapori hayo.
Aidha kutokana na hofu hiyo ya Usalama kamati hiyo imetoa siku saba kwa wamiliki wa mapori hayo kuyasafisha mara moja na ifikapo August 15 mapori yote yasiosafishwa watapewa wananchi au kutengwa ili yatumike kwa shughuli za kijamii.
M/kiti wa Mtaa wa mji  mpya amemtaka Mkuu wa mkoa wa dsm Paul Makonda kufika eneo hilo ili ajionee hali ilivyo pamoja na waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi ili kuwanusuru na hofu inayowakumba.


No comments:

Post a Comment