Saturday 13 August 2016

Mwanamke abakwa, auawa na kutupwa kichakani Mkoani Dodoma.


MWANAMKE anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40, amekutwa amekufa katika mazingira yanayoonesha kwamba alibakwa kabla ya kuuawa na kutupwa kichakani.

Mwili wake ulionekana Agosti 10, mwaka huu saa 7.30 mchana katika Kijiji cha Iringa Mvumi, Kata ya Mvumi, Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema kwamba wanamfanya msako waliotenda unyama huo ili wawafikishe katika mkondo wa sheria.

Alitoa mwito kwa wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi na vijiji vya jirani kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwafichua wahalifu hao ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Wakati huo huo, Mahakama ya Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma imemtupa jela miaka 30 mkazi wa Kijiji cha Mlali Iyengu, Mkengela Mchechele (27) baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 11.


No comments:

Post a Comment