Sunday 14 August 2016

Rais mstaafu wa awamu ya pili Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia leo.




Rais mstaafu wa awamu ya pili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia leo saa saba mchana nyumbani kwake katika kijiji cha Mji Mwema, eneo la kigamboni jijini Dar es salaam.


Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud, mwili wa Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambaye pia alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kusafirishwa kesho kwa ndege kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya maziko.
Amesema Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo la Migombani, Mkoa wa Mjini Magharib mnamo saa saba za mchana.

Aidha viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kuhudhuria maziko hayo ya Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambaye alikuwa Rais wa Zanzibar tangu mwaka 1972 hadi alipojiuzulu mwaka 1984.

USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment