Sunday 14 August 2016

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atoa tamko hili kuhusu uchaguzi mkuu wa Zambia.


Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete leo ametoa tamko la Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola  la Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika tarehe 11 Agosti, 2016 kuchagua Rais, Wabunge, Mameya, Madiwani na Kura ya Maoni ya Katiba. 

Rais Mstaafu Kikwete yuko nchini Zambia kufuatia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kumteua kuwa Mwenyekiti wa Timu hiyo yenye waangalizi wa kimataifa 17 kutoka nchi za Jumuiya ya Madola.

Kwa mujibu wa tamko hilo, Jumuiya ya Madola imejiridhisha kuwa zoezi la upigaji kura, usimamizi wa kura na uhesabuji kura vituoni kwa ajili ya umeendeshwa kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni bora za uendeshaji wa chaguzi.

 Tamko linasema, dosari na hitilafu zilizojitokeza hazikuwa kubwa kiasi cha kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu huo.

Amewapongeza wananchi wa Zambia kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa amani na kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka. 

Amewasihi viongozi wa kisiasa wa Zambia, wagombea na vyama vya siasa kuheshimu maamuzi wa wananchi na pale inapojitokeza upande wowote kutoridhika na matokeo, zitumike njia za amani na kisheria za kutafuta ufumbuzi.


USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment