Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm Rais Dk. John Pombe Magufuli, ameapa kupambana na mafisadi waliopo ndani ya chama hicho ambao wamekuwa wakikwamisha maendeleo ya Chama huku pia akiwaonya wanachama kutowatetea pindi atakapoanza kazi hiyo.
Dk. Magufuli ambaye alikuwa akizungumza kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini DSM baada ya kuwasili kutoka ziara ya Kanda ya Ziwa, ameeleza kwamba anaamini kuchaguliwa kwake ndani ya ccm kuwa mwenyekiti, baadhi ya wanachama hawakupenda iwe hivyo kwa kuwa wanatambua atawabana kutokana na ufisadi wao wa kula mali za chama hicho.
Amewataka wanachama wa ccm, kuwa waandilifu, la sivyo watakutana na mkono wake kwa kuwa anatambua chama hicho kina wanachama wasiokuwa waminifu ambao wamefilisi mali za ccm.
Aidha amewatoa wasiwasi wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla juu ya Serikali kuhamia Dodoma huku jiji la Dar es Salaam, likibaki kuwa jiji la kibiashara pekee.
Awali akimkaribisha Mwenyekiti huyo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhaman Kinana, alisema kuwa kazi kubwa ndani ya chama hicho ni kuhakikisha wananchi wanapata haki za kimaendeleo hususani vijijini, huku Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisistiza kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo Machinga wanapaswa kufuata sheria katika sehemu za kufanyia biashara.
USISAHAU KULIKE NA KUSHARE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPA ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment