Thursday 8 September 2016

Hospitali ya Dodoma yaanza kutoa huduma kwa wagongwa wa saratani kwa watoto wadogo kwa mtindo huu.

Image result for hospitali ya mkoa dodoma
Hospitali ya Benjamin Mkapa ya UDOM, Mjini Dodoma imeanza kutoa huduma ya ugonjwa wa saratani kwa watoto wadogo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la marafiki wa watoto wanaoishi na saratani nchini.


Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. James Charles, amesema kuwa hospitiali hiyo itatoa huduma kwa kutumia taarifa za wagonjwa kutoka katika vituo vya afya.

Dkt. Charles amesema kuwa kuanza kwa kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia wakazi wa Dodoma na mikoa ya kati kuanza kupata matibabu hayo kwa wakati huku akizitaja dalili za saratani kwa watoto wadogo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika hilo la marafiki kwa watoto wanaoishi na saratani, Janeth Malone, amesema kuwa tafiti zinaonesha kuwa zaidi ya watu elfu 40 kila mwaka wanapata saratani nchini Tanzania.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment