Thursday 8 September 2016

Mkutano wa viongozi wa EAC kufanyika leo jijini Dar es salaam.

Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wakiwa na mwenyekiti wa EAC, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli

Mkutano wa Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,(EAC) unafanyika hii leo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo marais wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wanatarajiwa kuhudhuria.

Mkutano huo una lengo la kujadili namna ya kutekeleza mkataba wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Ulaya(EPA).

Mkutano huo wa viongozi wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, unatarajiwa kuhudhuriwa na mwenyeji wa mkutano huo Rais Dkt. John Magufuli, Rais Yoweri Museven wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na nchi nyingine zitawakilishwa na mawaziri.

Wakati mkutano huo ukitarajiwa kuanza tayari nchi za Kenya, Rwanda na Uganda, zimekwishasaini mkataba huo wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara huku Tanzania ikikataa kufanya hivyo kwa madai kuwa mkataba huo utaizuia nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda kwa kukuza uchumi wake.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment