Monday 5 September 2016

Mgogoro ndani ya chama cha CUF wafika hapa,Julius Mtatiro anena haya.

Image result for Julius Mtatiro
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi iliyopewa jukumu la kusimamia kwa muda shughuli za Chama cha Wananchi CUF Bw. Julius Mtatiro 
Fukuto la mgogoro ndani ya Chama cha Wananchi CUF limeendelea ikiwa ni siku chache baada ya chama hicho kuwasimamisha uongozi baadhi ya wanachama, ambao nao waliibuka na kupinga kusimamishwa kwao.

Kundi linalomuunga mkono aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba na ambalo huendesha harakati zake kupitia makongamano ya kuhuisha chama hicho upande wa Tanzania Bara, limevamia makao makuu ya chama hicho kwa lengo la kuzuia mkutano na wanahabari uliokuwa unafanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni jijini Dar es Salaam.

Kiongozi wa Kundi hilo Bw. Miraji Mtibwiliko amewaambia wanahabari kuwa hatua yao hiyo inalenga kuutaka uongozi wa muda wa CUF kuheshimu agizo lililotolewa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa linalozitaka pande zote zinazopingana ndani ya chama hicho kutojihusisha na shughuli za chama hadi pale Msajili atakapotoa uamuzi wa barua ya pingamizi iliyowasilishwa katika ofisi hiyo na Profesa Lipumba.

Kitendo hicho kililazimu Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi katika ofisi za chama hicho, huku Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi iliyopewa jukumu la kusimamia shughuli za chama kwa muda Bw. Julius Mtatiro akikana kuwepo kwa mgogoro kwa madai kuwa chama chao bado ni imara tofauti na ambavyo imekuwa ikidaiwa.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment