Monday, 5 September 2016

Serikali yatoa Msisitizo huu kuhusu mpango wa utekelezaji wa ujenzi wa viwanda nchini.

Image result for Jenista Mhagama
Serikali inataka kuona ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, mpango wa mifuko ya hifadhi ya jamii katika ujenzi wa viwanda nchini, unaanza kutekelezwa kwa vitendo badala ya kuendelea kuwa wa maneno matupu.

Msisitizo huo wa serikali umetolewa mjini Dodoma na waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Bibi. Jenister Mhagama, wakati serikali ilipokuwa ikipokea taarifa ya mpango wa utekelezaji kutoka kwa mashirika mbalimbali ya hifadhi ya jamii, yaliyopo nchini.
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijage amesisitiza kuwa hakuna jambo lililopangwa kwa kukurupuka, kuwapa jukumu la ujenzi wa viwanda, mashirika hayo ya hifadhi ya jamii.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, jinsi mpango huo utakavyotekelezwa, Katibu Mkuu wa Chama cha mashirika hayo ya hifadhi ya jamii (TSSA), Bw. Meshach Bandawe, amesema viwanda vitakavyojengwa na shirika moja moja na vingine vitajengwa kwa kushirikiana.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment