Naibu Waziri wa nchi -Tamisemi Seleman Jaffo amefanya ziara ya Ukaguzi katika shule mbalimbali za wilayani Temeke ili kuona mafanikio yaliyopatikana katika kukabiliana na Upungufu wa madawati pamoja na madarasa ambapo amepongeza jitihada zinazofanywa kupitia kituo cha chanel ten kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kufanikisha upatikanaji wa madawati .
Aidha Naibu waziri Jaffo amekabidhi madawati 400 katika Shule ya Msingi Chemchem ,pamoja na kutoa maelekezo ya ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi nzasa pamoja na kuagiza ukarabati wa madarasa matano katika shule hiyo.
Akizungumza baada ya kutembelea shule hizo, Bwana jaffo amesema upatikanaji wa Madawati katika shule za msingi ambazo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto hiyo wilayani Temeke kwa sasa unaridhisha. Amewataka Mkuu wa wilaya hiyo na viongozi wa manispaa kuelekeza nguvu katika kuhakikisha wanakabiliana na Upungufu wa madarasa.
Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke Naseeb Mbaga amesema Wanaendelea na Utekelezaji wa maagizo ya Naibu waziri ambapo manispaa hiyo kupitia mapato yake ya ndani imeendelea kuboresha miundombinu katika shule hizo.
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA
ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment