Monday, 10 October 2016

Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako atoa siku 14 kwa Katibu Mkuu kuhusu kupata Taarifa ya ujenzi wa Chuo cha Ualimu Mtwara.

Image result for Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amemtaka Katibu Mkuu wa wizara hiyo kufanya uchunguzi  ndani ya siku kumi na nne kubaini sababu za kuchelewa kuanza kwa ujenzi wa Chuo cha Ualimu cha Kitangari kilichopo wilaya ya Newala mkoani Mtwara na kwa nini unachukua muda mrefu .

Waziri Ndalichako ametembelea chuo hicho na kusikitishwa na kasi ya ujenzi ambapo ameonya kuwa waliohusika kuchelewesha mradi huo watachukuliwa hatua za kisheria.
Chuo cha ualimu cha Kitangari ambacho kwa miaka miwili kimefungwa na kusitishwa kuchukua wanafunzi kutokana na miundombinu kuwa mibovu kimetengewa zaidi ya shilingi bilioni nane ili kukarabati na kujenga majengo mapya,lakini pamoja na jitihada hizo ujenzi umekuwa ukisuasua.
Awali akitoa taarifa kwa waziri huyo,mkuu wa wilaya ya Newala Aziza Mangosongo amezungumzia changamoto zilizopo katika mradi huo,hali iliyomlazimu waziri kuwataka wakandarasi kuheshimu mamlaka.
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment