Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo
tarehe 10 Oktoba, 2016 amepokea hati za
utambulisho za mabalozi wanne
wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi waliowasilisha hati zao za
utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni
Balozi wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini
Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi,
Balozi wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini
Mhe. Frantisek Dlhopolcek, Balozi wa
Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni
Tsymbaliuk na Balozi wa Jamhuri ya Ghana
Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam |
Rais Magufuli amezungumza na Mabalozi
hao kwa nyakati tofauti baada ya kupokea
hati zao za utambulisho, ambapo
wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza na
kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya
Tanzania na nchi hizo kwa kujikita zaidi
katika biashara na uwekezaji.
"Mhe. Balozi najua nchi yenu ya Sudan ina
utajiri wa mafuta na imefanikiwa kujenga
uchumi wake kupitia mafuta, sisi pia hapa
nchini tumebaini uwepo wa mafuta na gesi
asilia katika maadhi ya maeneo,
ningependa uhusiano na ushirikiano wetu
sasa ujielekeza katika kubadilishana uzoefu
na ujuzi wa namna tunavyoweza kunufaika
na mafuta na gesi" amesema Rais
Magufuli
alipokuwa akizungumza na Balozi wa
Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed
Abd Allah Sharfi.
Dkt. Magufuli pia ametoa wito kwa
wafanyabiashara na wawekezaji kutoka
nchi za Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana
kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta
mbalimbali zikiwemo Mafuta na gesi,
Kilimo,
Uvuvi, Mbuga za wanyama, Madini na
ufugaji.
"Hivi sasa Tanzania ipo katika mpango wa
ujenzi wa viwanda na pia tunatekeleza
mpango wa pili wa maendeleo, hivyo
nakuomba Mhe. Balozi uwahamasishe
wafanyabiashara na wawekezaji wa
Ukraine
waje wawekeze katika viwanda kwani soko
la uhakika la bidhaa lipo"amesisitiza Dkt.
Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi
wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni
Tsymbaliuk.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ukraine |
Aidha, Rais Magufuli amewasihi Mabalozi
wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao
makazi yao ya Ubalozi yapo Mjini Nairobi
nchini Kenya kuanzisha Ubalozi wao hapa
nchini ili kuimarisha zaidi uhusiano na
ushirikiano katika masuala ya biashara na
uwekezaji.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia Frantisek Dlhopolcek |
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Oktoba, 2016
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA
ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment