Monday, 10 October 2016

Haya ndio aliyoyazungumza Beki wa zamani wa Yanga Mwalusako kuhusu mabadiliko wanayotaka kufanya yanga.

Image result for Lawrance Mwalusako
Beki wa zamani wa Yanga, Lawrance Mwalusako amewashukia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kuwataka wawe makini katika suala la mabadiliko wanayotaka kufanya Yanga.

Mwalusako ambaye pia aliwahi kuwa katibu mkuu wa Yanga, amewaambia BMT kuwa, kuendesha timu gharama na wajue Yanga wameridhia wenyewe.

Hivi karibuni, BMT kupitia Katibu wake, Mohamed Kiganja imeibuka na kuyazugumzia mabadiliko ya Yanga kutaka kukodisha inagwa imeonekana kujichanganya sana katika hilo kwa kuwa mengi inayotaka yafanyiwe kazi, yaliishafanyiwa kazi.

“Katika hili BMT naona hawapo sawa kwa sababu Yanga ina haki yake ya kujiamulia mambo yake kwa ajili ya manufaa yake.

“Inashangaza sana kila linapokuja jambo fulani BMT wanaingilia lakini katika michezo mingine hawafanyi hivyo wakati huko ndiko kuna madudu mengi.

“Hakika hii siyo sawa kwani kuendesha timu siyo jambo rahisi hata kidogo, mimi nimekuwa kiongozi pale Yanga, najua matatizo yaliyomo ndani ya klabu hiyo yanayohusu uchumi, sasa kapatikana mtu ambaye atasaidia mambo kuwa sawa tunampinga! Katika hili siwaungi mkono BMT.


“Waliokuwa wanatakiwa kupiga kelele ni TFF, Caf na Fifa ambao ndiyo wenye jukumu la kusimamia soka kama mfumo huu wa kukodishwa timu haufai na siyo BMT.”

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment