Mkurugenzi wa Elimu na huduma kwa mlipa kodi wa TRA, Bw. Richard Kayombo amesema mwenendo wa ukusanyaji mapato ya Serikali kwa sasa ni wa kuridhisha katika kufikia lengo la kukusanya kiasi cha shilingi trioni 15.1 kwa mwaka fedha wa 2016/2017.
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imekusanya Mapato ya shilingi trilioni 1.37 kwa Mwezi September kati ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.4 mwezi huo
Kuhusu zoezi la uboreshaji wa taarifa ya namba za utambulisho wa mlipa kodi linaloendelea jijini Dar es Salaam, Bw. Richard Kayombo amesema mpaka sasa TRA imetoa vyeti vipya vya TIN kwa watu 15, 467 na zimebaki siku tisa kukamilisha zoezi hilo.
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA
KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA
ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment