Friday, 7 October 2016

Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof Lipumba kuanza ziara ya nje ya nchi kwa muda wa wiki mbili


Image result for Mwenyekiti wa Chama cha CUF
Mwenyekiti wa Chama cha CUF Pro Lipumba wiki ijayo ataanza ziara ya wiki mbili kutembelea mataifa kadhaa yakiwepo Ujerumani, Uingereza na Uholanzi.

Akiwa huko Pro Lipumba atapata fursa ya kufungua matawi ya CUF na kuzungumza wapenzi wa CUF na watanzania waishio nje ya nchi.

Pia Lipumba atapata fursa ya kukutana na Viongozi kadhaa wa mataifa hayo na kuzungumzia demokrasia na hali ya siasa inayoendelea Tanzania .

Pro Lipumba katika ziara hiyo atafuatana na maafisa kadhaa wa CUF wakiwepo wabunge Magdlena Sakaya na Mheshimiwa Maftah,
Wajumbe wengine ni waheshimiwa wajumbe 4 wa Baraza Kuu kutoka Zanzibar na Tanzania bara.

Pia Prof Lipumba atafuatana na wadhamini watatu wa Chama kuangalia uwezekano wa CUF kupata ufadhili kutoka kwa marafiki nje ya nchi.
Haki sawa kwa wote.

Imetolewa na:
Abdul Kambaya 
Mkurugenzi wa habari na Mawasiliano ya umma

No comments:

Post a Comment