Samsung imetoa wito kwa watu wenye simu aina ya Galaxy Note 7 kuzizima mara moja huku ikifanya uchunguzi kubaini ni kwa nini simu hizo, hata zile ambazo kampuni hiyo ilikuwa imethibitisha kwamba ni salama, zinawaka moto.
| Muonekano wa Samsung Galaxy Note 7. |
Kampuni hiyo ya Korea Kusini imesema itasitisha uuzaji wote wa simu hizo.
Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.
Walipewa simu mpya ambazo zilidaiwa kuwa salama.
Lakini sasa taarifa zimetokea kwamba hata simu hizo zilizodaiwa kuwa salama zinashika moto.
| Simu ya Samsung Galaxy note 7 iliowaka moto |
Mwanamume mmoja jimbo la Kentucky, Marekani anasema aliamka na kupata chumba chake cha kulala kimejaa moshi uliotokana na simu mpya ya Note 7 aliyokuwa ameipata baada ya kurejesha ya awali.
Siku chache awali, abiria kwenye ndege moja Marekani walitakiwa kuondoka kwa dharura ndegeni baada ya simu ya Note 7 kuanza kutoa moshi.
"Kwa sababu usalama wa wateja ni jambo tunalotilia maanani zaidi, Samsung itawataka wasambazaji wote na wauzaji wake kote duniani kusitisha uuzaji na pia ubadilishaji wa simu za Galaxy Note 7 uchunguzi unapoendelea," kampuni hiyo imesema
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA
ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment