Shirikisho la soka nchini TFF, limetoa
msimamo wake kuhusu suala la klabu ya
Yanga kukodishwa kwa muda wa miaka kumi
kwa kampuni ya Yanga Yetu.
Katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika mapema hii leo, katibu mkuu wa
TFF Celestine Mwesigwa amesema shirikisho
halijapata taarifa yoyote kuhusiana na
mabadiliko yoyote katika klabu ya Yanga
licha
ya kusoma taarifa hizo katika vyombo vya
habari.
Mwesigwa amesema TFF bado inatambua
hadhi ya Yanga kubaki vilevile hadi
watakapopewa taarifa rasmi na uongozi wa
klabu hiyo na kuzipitia ili kuhakikisha kama
kanuni na taratibu za TFF, CAF na FIFA
zimefuatwa.
‘Nimewaandikia klabu ya Yanga watupe
nakala za mkataba wa ukodishwaji
watuelezee nini kimeuzwa, kipi
kimekodishwa. Kwa sasa msimamo wa TFF
ni kuwa hadhi ya Yanga iko pale pale.’
TFF wametangaza msimamo huo ikiwa ni
siku kadhaa baada ya baraza la michezo la
taifa BMT, kuwataka Yanga kufuata taratibu
za kikatiba ili kukamilisha mchakato ambao
umedhamiriwa kufanywa kupitia bodi ya
wadhamini na uongozi wa kampuni ya Yanga
Yetu ambayo ipo chini ya mwenyekiti Yusuf
Manji.
Katibu mkuu wa BMT Mohamed Kiganja,
alieleza wazi kuwa mchakato wa kukodishwa
kwa klabu ya Yanga ni batili kutokana na
suala hilo kutokuwa na baraka za mkutano
mkuu wa wanachama na pia bodi ya
wadhamini ambayo inadaiwa kusaini
mkataba
wa kukodishwa aliita kuwa ni batili kufuatia
kuwa na wajumbe wasiotambulika kisheria.
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA
ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment