Tuesday, 11 October 2016

TFF yatoa tamko hili kuhusu hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya kiungo Mussa Ndusha


Image result for SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limewatuliza Simba SC kuhusu Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya kiungo Mussa Ndusha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), likisema inaweza kuwasili wakati wowote kuanzia sasa.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas Mapunda aliiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana kwamba wamewasiliana na Shirikisho la Soka DRC kuhusu ITC ya Ndusha na wamesema wanatuma.

“Yaani sisi tunawasubiri wao tu watume, wamesema wanatuma. Wakati wowote ikitumwa tutawapa Simba leseni waanze kumtumia,”alisema Mapunda.



Ndusha ni mchezaji pekee wa kigeni ambaye Simba imemsajili msimu huu, lakini imeshindwa kumtumia kutokana na kuchelewa kwa ITC yake.

Wachezaji wengine wa kigeni wa Simba SC ni kipa Vincent Angban, mshambuliaji Frederick Blagnon wote raia wa Ivory Coast, mabeki Juuko Murshid kutoka Uganda, Janvier Besala Bokungu kutoka DRC, Method Mwanjali kutoka Zimbabwe na washambuliaji Laudit Mavugo kutoka Burundi.

Ndusha yumo mjini Mbeya na kikosi cha Simba SC ambako wamekwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mbeya City. 


USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

No comments:

Post a Comment