Thursday 3 November 2016

Hii ndio sababu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa kibali cha Tundu Lissu kukamatwa.

Image result for Tundu lissu mahakamani
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imetoa amri ya  kukamatwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kuamuru wadhamini wake kufika mahakamani hapo kujieleza kwanini wasilipe fungu la dhamana kutokana na mshtakiwa huyo kushindwa kufika kusikiliza kesi yake bila ruhusa.


Lissu na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio.

Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa kesi hiyo ilipangwa jana kutajwa lakini mshtakiwa wa nne Lissu hakuwepo mahakamani.

Hata hivyo, alijitokeza mdhamini wake mmoja kati ya wawili Robart Katula kudai kuwa mshtakiwa huyo anaendesha kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Mwanza.

Hakimu alihoji kwa nini mshtakiwa amesafiri na kuacha kuhudhuria kesi yake bila kuomba kibali cha mahakama yake.

"Mshtakiwa Lissu anafanya dharau  kila wakati inapopangwa kesi yake mahakamani anashindwa kuhudhuria bila kutoa sababu ama kuomba ruhusa ya mahakama... kama asingekuwa nje kwa dhamana angefanyaje? angetumia busara kuomba ruhusa" alihoji na kuongeza kuwa.

"Wadhamini wa mshtakiwa wapelekewe wito wa mahakama waje kujieleza kwanini wasilipe fungu la dhamana kama walivyoahidi kwenye hati ya dhamana ya maneno ya Sh. milioni 10 kila mmoja" alisema Hakimu Simba.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Patrick Mwita aliomba mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa mshtakiwa.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

                          SUBSCRIBE ON YOUTUBE TIKISA TV

No comments:

Post a Comment