Saturday 26 November 2016

HIVI PUNDE:Rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro afariki dunia.

Image result for Fidel Castro
Fidel Castro, kiongozi wa zamani wa Cuba aliyeongoza mapinduzi ya Kikomunisti, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, kakake ametangaza.

"Amiri jeshi mkuu wa mapinduzi ya Cuba alifariki dunia mwendo wa saa 22:29 usiku huu (03:29 GMT Jumamosi)," Rais Raul Castro ametangaza.
Fidel Castro alitawala Cuba kama taifa la chama kimoja kwa karibu miaka 50 kabla ya kakake Raul kuchukua hatamu 2008.
Wafuasi wake walisema alikuwa ameirejesha Cuba kwa wananchi.
Lakini alituhumiwa pia kwa kuwakandamiza wapinzani.
Chini ya uongozi wa Fidel Castro, Cuba ilikuwa na uhusiano maalum na Afrika.
Katika miaka ya 1970 na 80, maelfu ya madaktari na walimu walikwenda Afrika na idadi sawa ya askari wa Cuba walipelekwa huko kuingilia kati migogoro na wakala wa vita baridi hasa nchini Angola.
Akitoa tangazo la kifo cha kakake, Rais Castro, aliyeonekana kuhuzunika sana, aliambia taifa kwenye tangazo la moja kwa moja kupitia runinga usiku kwamba Fidel Castro alikuwa amefariki na mwili wake utachomwa Jumamosi.
Kutakuwa na siku kadha za maombolezo ya kitaifa katika kisiwa hicho.

Raul Castro alihitimisha tangazo lake kwa kutamka kauli mbiu ya mapinduzi ya Cuba: "Twaelekea kwenye ushindi, daima!"

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE



                                SUBSCRIBE ON YOUTUBE 
                                          
                                               TIKISA TV

No comments:

Post a Comment