Saturday, 26 November 2016

Alichokizungumza Mama Maria Nyerere kuhusu kifo cha Rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro.


Image result for mama maria Nyerere
Baada ya Serikali ya CUBA kutangaza kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo FIDER CASTRO kilichotokea leo,mjane wa baba wa taifa mama Maria Nyerere amepokea kwa masikitiko makubwa kifo hicho cha mwanamapinduzi huyo.


Akizungumzia msiba huo mama maria Nyerere amesema CUBA na Dunia nzima ikiwemo Tanzania imepoteza mtu muhimu sana katika mambo ya kupigania haki,usawa na demokrasia.

Amesema wakati wa harakati mwaka wa 1973 Fider Castro alikutana na mwalimu na kujadili mambo mbalimbali kuhusu ukombozi wa bara la afrika pamoja na nchi ambazo hazikuwa huru wakati huo.
Mama Maria Nyerere anampa pole,rais wa nchi hiyo,familia ya hayati Castro pamoja na wananchi wote wa nchi ya Jamhuri ya watu wa CUBA.

Mama Maria Nyerere amesema msiba huo umewagusa si wananchi wa CUBA bali hata watanzania pia umetugusa kutokana na msaada ambao Fider Castro aliutoa kwa nchi yetu kwa kushirikiana na hayati baba wa taifa mwalimu Julius kambarage Nyerere

Fidel Castro na mwenyeji wake Hayati Mwalimu Nyerere akipokea heshima ya kijeshi alipowasili Dar Es Salaam Machi 1977.

Kwa upande wake Mbunge wa Afrika Mashariki Charles Makongoro Nyerere naye ameungana na Mama Maria Nyerere kwa kutoa salamu za pole kwa wananchi wan chi hiyo pamoja na kiongozi mkuu wake.

Amewataka wananchi wa CUBa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu kwa kuwa hayo ni maamuzi ya Mwenyezi Mungu yapaswa kushukuriwa.

Imetolewa na

MAKONGORO NYERERE
MBUNGE AFRIKA MASHARIKI.


USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE




                                SUBSCRIBE ON YOUTUBE 
                                          
                                               TIKISA TV

No comments:

Post a Comment