Wednesday, 30 November 2016

Mahakama yatoa maamuzi kuhusu kesi ya maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Kesi inayowakabili waliokuwa maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Martin Chacha na Juma Matandika iliyosomwa leo Jumatano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, imesogezwa mbele ambapo sasa itasikilizwa tena Desemba 5, mwaka huu.
 
Chacha na Matandika wanakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya shilingi milioni 25 kutoka kwa viongozi wa timu ya Geita Gold ya Geita kwa ajili ya kuwasaidia kuwapandisha daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza hadi Ligi Kuu Bara.



Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Huruma Shaidi, ilisomwa leo Jumatano ambapo upande wa mashtaka shahidi Sosthenes Kibwengo ambaye ni Mchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) alitoa ushahidi juu ya watuhumiwa hao kuomba fedha hizo kwa viongozi wa Geita, Salum Kulunge na Constastine Molandi ambapo aliwasilisha ushahidi wa sauti iliyopo kwenye CD ambayo ilisikilizwa na hakimu huyo.
 
Lakini upande wa washtakiwa, wameomba kesi hiyo isogezwe mbele hadi Jumatatu ijayo ya Desemba 5, kwa ajili ya kuja kumuhoji kwa kina shahidi huyo.


USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE




                                SUBSCRIBE ON YOUTUBE 
                                          
                                               TIKISA TV

No comments:

Post a Comment