Profesa Einar Svastard ( kulia) akimkabidhi msaada wa mashine kubwa ya kisasa ya Utrasound Mkurugenzi wa huduma za tiba MNH Dk. Hedwiga Swai. |
Msaada huo umetolewa jana na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha nchini Norway ambapo pamoja na mambo mengine wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika maeneo ya elimu , utafiti pamoja na vifaa tiba.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo ambaye pia Mhadhiri kutoka MUHAS Paschal Ruggajo amesema mashine hiyo itasaidia kuchukua sampuli ya figo kwa ajili ya kugundua magonjwa ya Figo , kuweka vifaa kwenye mishipa damu kwa wagonjwa wanaoanzishiwa matibabu ya uchujaji wa damu na kugundua matatizo mbalimbali ya Figo.
“ Kwa muda mrefu sasa tumekua na ushirikiano wa karibu kati ya Hospitali hiyo , MUHAS na MNH na wametusaidia kufundisha Madaktari sita wa Figo , wameshatoa mashine za kusafisha Figo na sasa wametupatia mashine hii kubwa ya Utra Sound kwakweli tunawashukuru kwa msaada wao.” Amesema Dk. Ruggajo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Dk . Hedwiga Swai ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba ameishukuru Hospitali hiyo ya Haukeland na kusisitiza kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka kwakua mashine hiyo itasaidia sana katika kitengo cha Figo
Profesa Einar Svastard akimfanyia uchunguzi mgonjwa kwa kutumia mashine hiyo.
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment