NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Jumatano kujiunga na kikosi cha timu hiyo kwa ajili yaa mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe mwishoni mwa wiki.
Samatta amesema kwamba anaondoka leo Genk, Ubelgiji kupitia Dubai ambako atalala siku mbili kabla ya kuunganisha safari ya kuja Dar es Salaam.
Samatta ameendelea kuonyesha umuhimu wa kuichezea Taifa Stars kwa kuitikia wito wa kocha Charles Boniface Mkwasa licha ya kuwa na majukumu mazito katika klabu yake.
Wachezaji 24 walioitwa na Mkwasa kwa ajili ya mchezo huo wa Novemba 13 mjini Harare, wataingia kambini Novemba 7, mwaka huu.
Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’ wa Yanga, Said Kipao wa JKT Ruvu na Aishi Manula wa Azam FC.
Mabeki; Erasto Nyoni, David Mwantika wa Azam FC, Michael Aidan wa JKT Ruvu, Mwinyi Hajji, Vincent Andrew wa Yanga, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba SC na James Josephat wa Prisons.
Viungo wa kati ni Himid Mao wa Azam FC, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Jonas Mkude na Muzamil Yassin wa Simba SC, wakati viungo wa pembeni ni Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, Shizza Kichuya, Jamal Mnyate wa Simba SC na Simon Msuva wa Yanga.
Washambuliaji ni Ibrahim Hajib wa Simba SC, John Bocco wa Azam FC, Elius Maguli wa Oman Club, Thomas Ulimwengu aliyemaliza mkataba wake TP Mazembe ya DRC na kundoka mwezi uliopita, Omar Mponda wa Ndanda FC na Nahodha Mbwana Samatta wa K.R.C Genk ya Ubelgiji.
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment