Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, amewaambia Simba kwamba mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara wasahau kabisa kutesa kama ilivyokuwa mzunguko wa kwanza.
Msuva ambaye mpaka sasa ana mabao saba katika ligi hiyo, ameisaidia Yanga kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 33 nyuma ya Simba yenye 35, huku timu hizo zote zikipoteza michezo miwili mpaka sasa.
Msuva amesema kuwa, mzunguko wa pili watafanya jitihada zote kuhakikisha wanaipindua Simba kwenye nafasi hiyo na kuikamata wao mpaka mwisho wa msimu.
“Simba wamekaa nafasi yetu na nawaambia mzunguko wa pili tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha tunawatoa hapo, tukikaa sisi hatutoki mpaka msimu unamalizika kwani tumedhamiria kuutetea ubingwa wetu,” alisema Msuva ambaye ni Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara mwezi Oktoba.
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
SUBSCRIBE ON YOUTUBE
No comments:
Post a Comment