Friday, 4 November 2016

Taarifa kamili kutoka Wizara ya Fedha kuhusu hali ya Uchumi nchini.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amehitisha mjadala wa mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na muongozo wa kuaanda mpango wa bajeti ya serikali ya serikali kwa mwaka 2017 /2018.


Akijibu hoja hizo Dkt. Mpango amesema kuwa uchumi wa nchi uko vizuri akiainisha vielelezo kadhaa vinavyoonesha ukuaji wa uchumi kushuka, kwa mfumuko wa bei, kubadilisha fedha pamoja na mapato ya ndani.
Dkt. Mpango amesema kuwa uchumi wa taifa una vigezo vingi vinavyoonyesha ukuaji wa uchumi ikiwemo kuongezeka kwa pato la taifa ambapo kwa Tanzania linaonekana limekuwa kwa mwaka huu ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka jana.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji akatolea ufafanunuzi hoja za kusahaulika ambapo amesema sekta hiyo wameiangalia kwa kina kwa kuwa sekta ya kilimo ni muhimu kwa ukuaji wa viwanda nchini.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

                          SUBSCRIBE ON YOUTUBE TIKISA TV

No comments:

Post a Comment