Thursday 17 November 2016

Tazama Donald Trump alivyowasili kwa kushtukiza katika mgahawa New York.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump aliwashangaza wateja, na wanahabari wanaofuatilia safari zake, baada ya kujitokeza kwa kushtukiza katika mgahawa mmoja New York.

Wanahabari waliopewa kazi ya kufuatilia safari zake walibaki kushangaa kwani walikuwa wameelezwa kwamba angesalia nyumbani jioni hiyo.
Lakini badala yake, aliandamana na kundi ndogo la maafisa hadi kwenye mgawaha wa 21 Club katika mtaa wa Manhattan, mmoja wa migahawa anayoipenda sana.
Fan club: President-elect Donald Trump was met with a standing ovation from stunned diners at 21 Club on Tuesday
Rais mteule wa Marekani Donald Trump akishangiliwa na baadhi ya wateja.
Video zilizopigwa wakati wa kisa hicho Jumatano zinamuonyesha Bw Trump akiwasalimia wateja na kuwaambia kwamba atapunguza kodi wanayolipa kwa serikali.

Kuwasili kwake 21 Club kulijulikana baada ya mwandishi wa Bloomberg, Taylor Riggs, ambaye kibahati alikuwa ameenda kwenye mgahawa huo, alipakia kwenye Twitter ujumbe wa kusema kwamba Trump alikuwa amefika kwenye mgahawa huo. Hata hivyo, alikosea jina la eneo na badala yake akasema ilikuwa ni Keene.
Kwenye video, Bw Trum anaonekana akiwaambia wateja: "Tutapunguza kodi mnayolipa, msiwe na wasiwasi kuhusu hilo."
Kundi la wanahabari waliopewa kazi ya kufuatilia safari za rais huyo mteule, inadaiwa waliambiwa na msemaji wa Bw Trump, Hope Hicks, mwendo wa saa 18:45 kwamba alikuwa amekamilisha shughuli za siku na kwamba walikuwa huru kwenda nyumbani.
Dakika 45 baadaye, msafara mkubwa wa magari ulionekana ukiondoka kutoka afisi kuu ya Bw Trump kwa sasa katika jumba la Trump Tower. Msafara huo ulijumuisha magari zaidi ya kumi na gari la kubeba wagonjwa.
Riggs alipoandika kwenye Twitter, wanahabari walikimbia mgahawa wa Keene kabla ya kugundua kwamba alikuwa 21 Club.
Hawakuruhusiwa kuingia Trump na familia yake walipokuwa wanakula chakula cha jioni kabla ya kiongozi huyo kuondoka na kurejea Trump Tower saa 21:41.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

                              SUBSCRIBE ON YOUTUBE TIKISA TV

No comments:

Post a Comment