Friday 11 November 2016

Tazama jinsi Rais Magufuli pamoja na viongozi wengine wakiaga mwili wa Marehemu Joseph Mungai.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 10 Novemba, 2016 aliwaongoza viongozi na wananchi wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Waziri na mbunge Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joseph James Mungai katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Rais Magufuli Viongozi wengine waliofika kuuaga mwili wa Marehemu Mungai ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu,  Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu. Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Viongozi wengine mbalimbali wa Serikali na Siasa.

Joseph James Mungai alifariki dunia tarehe 08 Novemba, 2016 katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua ghafla na mwili wake utasafirishwa leo Ijumaa kwenda Mafinga Mkoani Iringa kwa Mazishi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na waombolezaji waliofika kuaga mwili wa Marehemu Joseph Muungai katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 10,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin Mkapa pamoja na waombolezaji  wengine walipofika kuaga mwili wa Marehemu Joseph Muungai katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 10,2016


USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

                              SUBSCRIBE ON YOUTUBE TIKISA TV

No comments:

Post a Comment