Wednesday 9 November 2016

Utabiri wa mhubiri maarufu TB Joshua kuwa Hillary Clinton atamshinda Donald Trump umegonga mwamba.

Image result for TB Joshua
Utabiri wa mhubiri maarufu raia wa Nigeria TB Joshua, kuwa Hillary Clinton atamshinda Donald Trump umeambulia patupu

Aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa Bi Clinton atashinda kwa kura chache. Kwa sasa ujumbe aliouandika kwenye mtandao umefutwa na sasa watu wanaendelea kumkejeli mhubiri huyo.
TB Joshua ni mmoja wa wahubiri maarufu na wenye kukumbwa na utata barani Afrika huku wengi wa wafuasi wake wakiamini kuwa utabiri wake ni wa ukweli.
Sawa na wahubiri wengine nchini Nigeria, TB Joshua ni tajiri na mwenye ushawishi mkubwa.
Watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia husafire hadi kanisa lake nchni Nigeria kutibiwa na kushuhudia unabi wake.
Wakati ugonjwa wa Ebola ulikumba eneo la magharibi mwa Afrika, mamlaka ya mji wa Lagos ilitangaza kuwa hakuna mgonjwa wa ugonjwa wa ebola angepelekwa kanisani humo kuponywa. Hii ilikuwa ni hatua ya kuzuia maambukizi
Baada ya kifo cha Michael Jackson, mhubiri huyo alidai kuwa hilo ni suala ambalo alikuwa amelizungumzia miezi sita kabla.
Lakini pia katika uchaguzi wa Tanzania uliofanyika oktoba 25 mwaka jana Muhubiri TB Joshua alimtabiria mgombea wa Chadema aliyekuwa  anawakilisha Umoja unaounda katiba ya wananchi UKAWA bwana Edward Lowassa kuwa atamshinda Rais Dk. John Magufuli jambo ambalo liligonga mwamba pia.
Wakosoaji wake wameutaja utabiri wake kuwa uongo. Hata hivyo hilo halijawazuia wafuasi wake kufurika kanisani mwake kutafuta mwelekeo.

USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

                              SUBSCRIBE ON YOUTUBE TIKISA TV

No comments:

Post a Comment