Wednesday 16 November 2016

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya umeme jijini Dar es salaam.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji umeme jijini Dar es salaam ambao utabadilisha taswira nzima ya upatikanaji wa huduma hiyo jijini humo na kuifanya kuwa ya uhakika zaidi.

Mradi huu unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 74.6 ambazo kati ya hizo bilioni 63.56 zimetolewa na serikali ya Finland huku Tanzania ikichangia bilioni 11.03.
Waziri Mkuu Majaliwa amebainisha kuwa kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa kwa wafanyabiashara kukamilisha azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kufungua viwanda ambapo vilivyopo vinashindwa kufanya kazi kutokana na kukosekana kwa nishati ya umeme ya uhakika lakini pia kutimiza ahadi ya serikali kupitia ilani ya chama cha mapinduzi kuwa itatoa umeme wa uhakika kwa wananchi na kufikia asilimia 75 mwaka huo.
Awali akizungumzia mradi huo waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo amelisisitizia shirika la umeme Tanzania Tanesco kwamba hatarajii kuona nchi inaingia katika mgao wa umeme au kukatika katika kwa umeme lakini pia utekelezwaji wa dhana ya Tanzania ya viwanda inahitaji umeme wa uhakika na gharama nafuu huku mkurugenzi mtendaji Tanesco Injinia Felchesmi Mramba akibainisha kuwa mradi huo utaweze kuunganisha vituo vyote vya umeme vya katika jiji la dar es salaam.
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

                              SUBSCRIBE ON YOUTUBE TIKISA TV

No comments:

Post a Comment