Wednesday 16 November 2016

Waziri Prof Makame Mbarawa amezindua Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli.

Image result for Prof Makame Mbarawa
Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa amezindua Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli ambapo ameipa changamoto kufanyakazi kwa bidii ili kulirudisha shirika hilo kwenye hali yake iliyokuwa zamani, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na upinzani unaotokana na malori yanayosafirisha malori.

Amebainisha kwamba inawezekana wafanyabiashara wa malori wanaliombea mabaya shirika hilo lidorore kama ilivyokuwa miaka michache iliyopita, ambapo amesisitiza huu ni wakati muafaka kwa bodi hiyo kuilekeza menejimenti kufanyakazi kwa uadilifu na kuondoa mgongano wa maslahi kati yao.
Aidha, Waziri huyo amewaomba kuachana na tabia iliyozoeleka ya wajumbe wa bodi kushiriki kwenye mambo ya kugawa zabuni na kusahau majukumu yao ambapo amesema Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa Reli ya ‘Standard Gauge’ itakayoharakisha usafirishaji wa abiria na mizigo.
Baadae waziri Mbarawa alikutana na wafanyakazi wa shirika hilo katika eneo la karakana ambapo alizungumza nao na kuwasisitizia umuhimu kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu kazini kwa kuacha vitendo vya wizi na ubadhirifu wa mali za umma.
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE

                              SUBSCRIBE ON YOUTUBE TIKISA TV

No comments:

Post a Comment