Baada ya kuwa katika uangalizi wa afya yake katika hospitali ya UCLA Medical Center, rapper huyo sasa amerejea nyumbani na mke wake Kim Kardashian kuungana na watoto wao, North na Saint.
West atakuwa chini ya uangalizi wa daktari wake, Michael Farzam. Huyu ndiye daktari aliyepiga simu ya 911 siku ambayo West alipelekwa hospitali, Novemba. 21.mwaka huu
Rapper huyo alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili yaliyochangiwa na uchovu, ukosefu wa usingizi na upungufu wa maji mwilini. Matatizo hayo yalipelekea kusitishwa kwa ziara yake ya Saint Pablo.
Kim Kardashian akiwa na Kanye West akitoka hospitali. |
Matatizo mengine yanayomsumbua rapper huyo ni msongo mkubwa wa mawazo, wasiwasi na huzuni ya kifo cha mama yake. Bado ataendelea na matibabu ya kisaikolojia na ya kawaida.
Hospitali ya UCLA Medical Center |
USISAHAU KULIKE NA KU-SHARE NA KU-LIKE PAGE YETU FACEBOOK TIKISA MEDIA KUFOLLOW TWITTER @TIKISA MEDIA NA INSTAGRAM TIKISA ENTERTAINMENT MEDIA ILI HABARI ZOTE KUBWA ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.ASANTE
No comments:
Post a Comment