Monday 9 January 2017

Maamuzi ya CHELSEA kuhusu kadi ya nyekundu aliyopewa John Terry.

Chelsea captain John Terry was sent off during the 4-1 FA Cup win over Peterborough United
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema klabu hiyo inatafakari uwezekano wa kukata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa nahodha John Terry wakati wa mechi ya FA Jumapili.

Chelsea walilaza Peterborough 4-1 mechi hiyo.
Blues walipokuwa mbele 3-0, Terry, 36, alimwangusha mshambuliaji Lee Angol na refa Kevin Friend akaamua kuwa alikuwa mchezaji wa mwisho wa Chelsea.
"Lazima uheshimu uamuzi, lakini wakati huu labda tutakata rufaa," alisema Conte.
Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Terry kuwa kwenye kikosi cha kuanza mechi tangu Oktoba.
Terry reacts to being sent off by referee Kevin Friend at Stamford Bridge on Sunday afternoon
Chelsea wakishindwa kwenye rufaa hiyo, basi Terry hatakubaliwa kucheza mechi ya Ligi ya Premia ugenini kwa mabingwa watetezi Leicester City tarehe 14 Januari.
John Terry ameoneshwa kadi tatu kati ya sita nyekundu walizoonyeshwa wachezaji wa Chelsea karibuni zaidi.

No comments:

Post a Comment