Tuesday 14 February 2017

Baada ya tuhuma ya Madawa ya kulevya, Uhamiaji nao waja kesi mpya kuhusu Yusuph Manji.


Yusuf-Manji-002.jpg
Yusuf Mehbub Manji ni mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Diwani wa Kata ya Mbagala kuu(CCM) Jimbo la Mbagala Dar es Salaam. Vilevile ni Mwenyekiti wa Club ya Mpira ya Nchini Tanzania Yanga Afrika SC
 Baada ya Sakata la Madawa ya Kulevya kumuandama mpaka kufikia kulazwa Hospitalini, Uhamiaji nao wamekuja na Mpya baada ya kukamata Passport 126 ofisini kwake za watu kutoka nje ambao wanafanya kazi kwenye kampuni yake bila vibali vya uhamiaji.

John Msumule ambaye ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam amesema, hii Kampuni ya Quality Group ipo katika jengo la Quality Center Barabara ya Nyerere kama unaelekea Uwanja wa ndege wa JNIA ni mkono wa kushoto. tumefanya kazi Ijumaa baada ya kuwekwa tu ndani yaani kesho yake jumamosi, tukapata Passport 126, Hizi ndizo zenye makosa. Tumechambua, passport 25 hawana vibali vya kufanya kazi, kwahiyo wanafanya kazi kinyume na utaratibu. Wote hawa hatua zitachukuliwa na watapelekwa Mahakamani.

Lakini lazima niseme ukweli, hawa hawatapelekwa peke yao mahakamani, lazima Yusuf Manji ambaye ndiye mwajiri wa watu hawa ambaye ndiye Mmliki wa Kampuni hii lazima afikishwe mahakamani kujibu shitaka la kuajiri watu wageni wasio na vibali. Jana tulikuwa tumkamate alale mahabusu na leo ndio tumpeleke Mahakamani, Bahati mbaya tulipokwenda kumkamata, tukaapewa taarifa kwamba amelazwa Hospitalini hadi sasa.

Mara tu atokapo, aripoti ofisi hii ili tumuunganishe kwenye kesi hii ya kuajiri watu wasio na vibali. Hatutajali ukubwa wa hela yako, hatutajali cheo chako cha mahali popote pale, hatutajali kwa njia yoyote ile una mamlaka gani katika nchi ya Tanzania.


No comments:

Post a Comment