Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
23 Machi, 2017 amefanya mabadiliko
madogo katika Baraza la Mawaziri.
Katika Mabadiliko hayo, Mhe. Rais
Magufuli
amemteua Prof. Palamagamba Aidan John
Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na
Sheria.
Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Dkt.
Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Uteuzi huu unaanza mara moja.
Wateule wote wataapishwa kesho Mchana
tarehe 24 Machi, 2017 Ikulu, Jijini Dar es
Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Machi, 2017
No comments:
Post a Comment