Tuesday, 20 June 2017

Ally Mayay Arejesha fomu yake kuelekea uchaguzi wa Rais mpya wa TFF




Ally Mayay anayewania Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amerejesha fomu.

Nahodha huyo wa zamani wa Yanga amerejesha fomu leo baada ya kuwa amechukua hiyo jana.


Pamoja na Mayay, mkongwe Mtemi Ramadhani naye amerejesha fomu ya kuwania nafasi ya umakamu wa TFF.


Mtemi, mmoja wa washambulizi hatari wa Simba enzi zake, aliambatana na Mayay kurejesha fomu hizo kama ambavyo walifanya jana wakati wakienda kuchukua fomu hizo.

No comments:

Post a Comment