Beki wa kushoto wa Azam, Gadiel Michael ambaye imeelezwa ameamua kuondoka, anaamini Yanga ndiyo sehemu sahihi ya yeye kuonyesha uwezo wake zaidi.
Tayari taarifa zinaeleza, Gadiel amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga.
“Yanga ni sehemu sahihi kwangu kwa maana ya ushindani na kukuza zaidi kiwango changu,” alisema.
Beki huyo alipendekezwa na Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina kwa ajili ya kumuongezea ushindani beki Haji Mwinyi kufuatia Oscar Joshua kumaliza mkataba wake.
No comments:
Post a Comment