Tuesday, 27 June 2017

Kichuya afunguka haya kuhusu Michuano ya Cosafa

Kichuya (kulia) akipambana na Fransis Mulimba wa malawi.



Baada ya kuanza vizuri michuano ya Cosafa kwa kupachika mabao mawili, Shiza Kichuya amesema anataka mabao zaidi.

Akihojiwa nchini Afrika Kusini, Kichuya amesema angependa kufunga mabao zaidi kutokana na nafasi zinavyopatikana.

“Mimi ni mchezaji ambaye ningependa kupata nafasi zaidi ya timu ya taifa. Kufunga mabao zaidi kutajenga imani zaidi kwa kocha lakini nitakuwa naisaidia timu.

“Kweli napenda kufunga zaidi, ikishindikana basi nitoe pasi nzuri zisaidie timu kucheza vizuri au kupata mabao,” alisema.


Kichuya alifunga mabao mawili katika mechi ya kwanza ya Taifa Stars wakati ilipoitwanga Malawi kwa mabao 2-0 na yeye kuibuka shujaa mwisho wa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment