Monday, 19 June 2017

Ukweli wa Ishu ya Haruna Niyonzima kuhusu kusaini Simba (+AUDIO)

Image result for haruna niyonzima
Taarifa za usajili wa kiungo Haruna Niyonzima, zimeendelea kuzua mjadala mkubwa mtandaoni.

Kuna wanaosema kasaini Simba na wengine wanadai ameongeza mkataba Yanga.

Habari kutoka kwa rafiki wa Niyonzima, zimeeleza hadi sasa kiungo huyo Mnyarwanda hajasaini upande wowote.

“Niyonzima hajasaini Simba wala Yanga, haya ni maneno tu ya watu ndugu yangu.  Lakini tutajua baadaye au siku nyingine,” kilieleza chanzo.

Niyonzima amekuwa akiwaniwa na Simba baada ya kuichezea Yanga kwa misimu sita akitokea APR ya Rwanda.

Msikilize Hapa mwenyewe

No comments:

Post a Comment