Friday 21 July 2017

Msuva aungana na Stars Rwanda.


Baada ya kukwama jijini Dar es Salaam, hatimaye Msuva ameondoka kwenda Rwanda kuungana na kikosi cha Taifa Stars.

Stars iko jijini Kigali kuivaa Rwanda  katika mechi ya kuwania kucheza michuano ya Chan. Katika mechi ya kwanza mjini Mwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Awali, Msuva alikwama kwenda Rwanda,  alifika hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JKIA), lakini baadaye alirejea nyumbani.

Lakini jana amefanikiwa kuondoka kwenda Rwanda kuongeza nguvu katika kikosi cha Stars.

No comments:

Post a Comment