Saturday 22 July 2017

Mtanzania akamatwa nchi india na Gram 300 za dawa ya kulevya.


2017_7$largeimg19_Wednesday_2017_010937986.jpg
Polisi katika mji wa Samrala wameripoti kumkamata Mwanamke, Mtanzania akiwa na gram 300 za Dawa za Kulevya aina ya Heroin.

Afisa wa Jeshi la Poisi, SSP- Khanna Navjot Singh Mahal amesema walipokua katika doria walimuona Mwanamke huyo akiwa amesimama huku ameshikilia begi dogo na mfuko wenye biskuti. Mwanamke huyo mara baada ya kuwaona Askari hao alianza kula Biskuti hizo, alipopekuliwa ndipo akabainika kuwa na Dawa hizo.

Mwanamke huyo baada ya kuhojiwa alidai kuwa anatokea Jiji la Delhi na anafanya kazi za mitindo katika hivyo alikuwa akipeleka Dawa hizo kwa ajili ya kuwauzia watu kadhaa kwenye mji wa Ludhiana.

No comments:

Post a Comment