Thursday 13 July 2017

Rais wa Brazil atoa msimamo wake kuhusu hukumu yake ya kifungo cha miaka 9 jela.

Image result for Luiz Inácio Lula da Silva
Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Ignacio Lula da Silva, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa na nusu jela miongoni mwa kesi tano za ulaji rushwa zinazomkabili.

Lula aliondoka kutoka umaskini enzi za utoto wake na kuwa mmoja wa marais maarufu zaidi wa Brazil
Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha muungano alijizolea umaarufu kutoka jamii ya kimataifa kwa sera zake za kijamii ambazo zilisaidia kuboresha maisha Brazil.
Lakini sasa mambo yamegeuka na kukutwa na hatia ya kukubali hongo ya zaidi ya dola milioni moja za malipo ya ghorofa ya mapumziko kwa ajili ya ukarabati wake kwa kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, iitwayo kwa kifupi OAS.
Hukumu hii inakuja wakati ambapo mtawala Lula akiwa ametoa msimamo mkali kwamba ana mpango wa kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais mwakani 
Kufuatia hukumu hiyo, rais huyo amekana mashtaka yote yanayomkabili kwa kudai kuwa hajafanya makosa yoyote kiasi cha kustahili hukumu hiyo, huku mawakili wanaomtetea wameapa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo

No comments:

Post a Comment