Kama unakumbuka tulikueleza kuhusiana na safari ya kiungo Ramadhani Singano maarufu kama Messi kwenda kujiunga na na klabu ya Difaa Al Jadida ya nchini Morocco.
Singano ameonekana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), tayari kwa safari ya kwenda Morocco.
Singano anakwenda kujiunga na Difaa Al Jadida ambayo tayari imesaini mkataba wake wa awali na atarejea nyumbani Tanzania Januari, mwakani kwa mapumziko.
Msimu uliopita, Al Jajida ilishika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Morocco maarufu kama Botola nyuma ya mabingwa, Raja Casablanca. Maana yake itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
No comments:
Post a Comment